Wa-Nuba waandamana Sudan

Maelfu ya waandamanaji wa Nuba kutoka Sudan walikuwa katika mji mkuu wa Khartoum, Jumatano wakipinga dhidi ya ghasia za karibuni za kikabila katika eneo lao la kusini mwa nchi.

Sudan ambayo imegubikwa na migogoro ya kisiasa na kiuchumi inashuhudia ongezeko zaidi la hali hiyo baada ya mapinduzi ya mwaka jana, na majeshi ya usalama kufanya msako mkali sana kwa takriban wiki nzima kwa wale wanaounga mkono demokrasia.

Taifa hilo la kaskazini mashariki mwa Afrika pia limekumbwa na mivutano kati ya makundi ya kiarabu na ya wale walio wachache yakiwemo mapambano ya mwezi uliopita ambayo yameua takriban watu 19 katika mkoa wa Kordofan Magharibi ambako wanuba wanaishi huko.

Takriban watu 19 waliuawa katika mji wa Lagawa mwezi uliopita muandamanaji mmoja Ahlam Ali, aliliambia shirika la habari la AFP.

Sisi ni wazawa kwahiyo wanataka kutulazimisha kuondoka kwenye ardhi zetu alisema muandamanaji mwingine, Saidi Issa.

Na kuongezea kuwa wanatumia nguvu ya dola na silaha zao lakini kamwe hatutakaa kimya.

Wanaharakati wanaounga mkono demokrasia mara nyingi wanawashutumu watawala wa kijeshi kwa kuchochea mivutano ya kikabila.

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, mwaka huu, zaidi ya watu 600 wameuwawa na zaidi ya 210,000 wamekoseshwa makazi kutokana na mizozo ya kikabila nchini Sudan.