Vyombo vya habari Uganda vina wanyima upinzani matangazo.

Kiongozi wa upinzani wa Uganda DK. Kizza Besigye akiwahutubia wafuasi wake huko Masaka Lyantonde, kiasi ya 200 kms magharibi ya Kampala mji mkuu wa Uganda, Nov. 6, 2010

Kampeni za uchaguzi mkuu huko Uganda zimeshika kasi kukiwepo wagombea wanane wa kiri cha Rais, katika uchaguzi unaotegemewa kufanyika Februari 18.

Viongozi wa upinzani wanalalamika kwamba vyombo vya habari nchi humo kwa sehemu kubwa vinakata kuwapatia nafasi kueleza sera na mismamo yao au kuzungumza na wapigaji kura hata ikiwa wako tayari kulipa fedha kununua muda wa matangazo.

Mwandishi habari wa gazeti la Daily Monitor, Don Wanyama, ameimabia Sauti ya Amerika kwamba ingawa kuna wagombea wanane wa kiti cha Rais, wagombea wanaonekana kuwa na ushindani mkuu ni Rais Yoweri Museveni, Dr Kizza Besigye, na Olara Otunnu.

Kwa upande mwengine siku ya Jumatano afisa wa cheo cha juu wa Mahakama ya Katiba alisema majina ya wagombea 70 wa viti vya bunge la Taifa yameondolewa kwa kutokamilisha masharti ya kushiriki katika uchaguzi.