Vyombo vya habari Kenya vyashutumiwa kuzoretesha maudhui ya jamii

Vyombo vya habari vyashutumiwa kuharibu maudhui ya jamii huko Kenya.

Utafiti wa halmashauri ya mawasiliano nchini Kenya kwa ushirikiano na shirika la utafiti la Momentrum Consulting Africa unaonesha kwamba wakenya saba kati ya 10 wanakhisi kuchukizwa na baadhi ya vipindi vya redio na televisheni nchini humo vinavyotoa ujumbe wa ngono na lugha zisizofaha kwa jamii hususan watoto wanapoangalia au kusikiliza matangazo hayo majira ya asubuhi na mchana.

Kwa mujibu wa utafiti huo halmashauri ina nia ya kudhibiti vipindi ambavyo haviendani na maadili au utamaduni wa jamii ili kuwalinda watoto wa kizazi hiki na cha baadae wasije wakaathirika katika masomo.

Mwandishi wa sauti ya Amerika-VOA mjini Nairobi, Kennedy Wandera alizungumza na baadhi ya wakenya kuhusu utafiti huo na kupata maoni na mtazamo wao.

Your browser doesn’t support HTML5

Ripoti ya Kennedy Wandera wa Nairobi, Kenya.

Aidha kwa mujibu wa sheria inayotarajiwa kuanza kufanya kazi mwezi huu halmashauri hiyo ilielezea njia mojawapo ya kudhibiti lugha zenye maneno makali kwa watoto wanapoangalia vipindi hivyo ni kupiga marufuku upeperushwaji wa vipindi hivyo kati ya saa kumi na moja asubuhi hadi saa nne usiku.

Utafiti huu umekuja wakati bodi ya kusimamia filamu na matangazo nchini kenya kuongeza maadili makali dhidi ya vyombo vya habari vinavyopeperusha filamu zinazoharibu maadili katika jamii.