Vyama vikuu vya siasa vya Nasa na Jubilee nchini Kenya vinaeleza katika ilani zao za uchaguzi mikakati yao katika kuboresha elimu nchini humo.
Kwa mujibu wa muungano wa Nasa wameahidi elimu bure ya msingi na kuzipa serikali za kaunti ruzuku za masharti .
Your browser doesn’t support HTML5
Jubilee nao wanasema wamelenga kubadili mfumo mzima wa elimu wa karne ya 21 kwa kufanya maamuzi yakutoa elimu ya bure kwa shule za kutwa nchini humo na upili.
“Na tukasema ya kwamba tunataka kuhakikisha ya kwamba hakuna mtoto tena ambaye atanyimwa nafasi katika chuo kikuu au katika shule ya sekondari ati kwasababu shule imesema ya kwamba wewe mzazi lipa mtihani ndio mtoto aweze apte cheti kitakachomwongoza.” alisema rais Uhuru Kenyatta.
Hali kadhalika muungano wa Nasa pia imeahidi elimu ya bure kuanzia chekechea mpaka sekondari.
Suala la elimu ya bure lilizungumzwa tangu wakati wa utawala wa rais Mwai Kibaki 2002 alipoahidi elimu ya msingi ya bure kwa wote nchini humo. Lakini ilikumbana na changamoto mbali mbali ikiwamo kufurika kwa wanafunzi wengi kupita idadi ya walimu, ada mbali mbali kama vile za ulinzi, majengo na mengineyo.
Katibu mkuu wa chama cha walimu nchini Kenya Wilson Sossionanaeleza jinsi NASA walivyopendekeza kushughulikia changamoto hizo ikiwamo ya upungufu wa walimu.
Anasema “ NASA wametuita na tumeweza kuketi na katika mapendekezo yao wamesema wataangalia maeneo mengine katika bajeti iliyopo kwa sasa na kusimamia bilioni 70 kwa mwaka ziende wizara ya elimu na kila mwaka wataajiri walimu 20,000 ndio katika kipindi cha miaka mine wapunguze upungudu wa walimu laki moja na tunaona hiyo inakwenda na idadi”.
Vyama vyote viwili vimetoa ahadi kwenye manifesto zao za elimu kuwa itakuwa ni ya bure. Lakini tunamulika ahadi hii na suala zima la elimu nchini Kenya ambalo limekumbana na changamoto nyingi za migomo ya elimu hasa kwa upande wa elimu ya juu.
Mkakati wa jubilee katika kuboresha elimu nchini humoni pia kuhakikisha kwamba watoto kuanzia chekechea hadi kufikia elimu ya sekondari wanapata elimu ya bure.
Na katika mkakati wa nasa wameeleza kwamba wanafunzi wapatao laki 2 na nusu wanakosa kwenda sekondari kila mwaka alieleza Musalia Mudavadi mmoja wa viongozi wa muungano wa Nasa. Naye Profesa Richard Basire wa chuo kikuu cha Nairobi bado anaona pande hizi mbili hazitofautiani.
Anasema “ukiangalia hawa wawili si tofauti vile manifesto zao kama ni sawa mmoja anasema ataanza wakati fulani na mwingine anasema ataanza wakati fulani lakini yote wanayoyasema ni yale yale tu”.
Je ahadi za chama cha Jubilee katika kuinua mfumo wa elimu nchini Kenya zinapokelewa vipi na chama cha walimu nchini humo, katibu mkuu wa chama cha walimu nchini Kenya Wilson Sossion anasema
“Kwa upande wa jubileeni sera ambayo tunaona ni ya kuhadaa wananchi kwasababu kutoa elimu ya sekondari kuna mambo kadhaa lazima yafanyike kwanza uajiri walimu wa kutosha kwasababu shule zetu za upili zina upungufu wa asilimia 37 ya walimu na hiyo ndio inaleta gharama isiyo ya moja kwa moja.”
Pia ikikukumbukwa kwamba kazi ya ualimu imekuwa ya hatari katika baadhi ya sehemu nchiniKenya na kutokana na miundo mbinu bado kuna watoto wanasafiri umbali mrefu kwa miguu kwenda shule, wengine kukosa chakula, wengine wakijifunza chini ya miti na usalama mdogo.
Je nini zaidi kingeweza kufanyika upande wa shule za bweni nchini humo katibu mkuu chama cha walimu anasema
“Hawajupatia suluhisho muafaka kwa miundo mbinu ya shule sababu ile inayovutia fensi ya juu ni mambo hayo kwa mashule hawajatupatia mfumo ambao tunaona kwamba inawezekana na inaweza kufanyika hawajatupatia mbadala wa mfumo wa chakula mashuleni sababu kwa shuke za bweni lazima kuwe na levi ya bweni halafu hawajupatia suluhisho sawa sawa la malipo ya katro na vifaa vya kujifunzia”.
Suala la elimu lina changamoto kubwa na vyama vyote viwili vikuu vimeazimia kuifanyia mabadiliko yanayopaswa.