Vurugu za wahamiaji na wenyeji Tunisia zasababisha kifo

Mtu mmoja nchini Tunisia ameuwawa katika mapigano kati ya wakaazi na wahamiaji kutoka nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara katika mji wa kusini wa Sfax, afisa wa mahakama amesema Jumanne, kufuatia siku za matukio ya vurugu kati ya wenyeji na wahamiaji.

Sfax, mji mkuu wa kiuchumi wa Tunisia, umejaa maelfu ya wahamiaji wa Kiafrika wanaotaka kwenda Ulaya kwa boti kutoka fukwe za pwani ya nchi hiyo katika msafara wa kuashiria mzozo wa wahamiaji ambao haujawahi kutokea katika nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Faouzi Masmoudi, msemaji wa mahakama ya Sfax, alisema polisi wamewakamata Waafrika watatu kutoka nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara wanaoshukiwa kuhusika na mauaji ya mtu huyo wa Tunisia siku ya Jumatatu.

Mauaji hayo yalifuatia usiku wa mapigano makali huko Sfax kati ya wakaazi na wahamiaji, aliongeza. Katika muda wa usiku mbili zilizopita, polisi walifytua gesi ya kutoa machozi kutuliza ghasia na mapigano.