Volker Turk anasema kipaumbele chake ni kumaliza vita vya Gaza

Volker Turk, Kamishna wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia haki za binaadamu. Picha na REUTERS/Denis Balibouse

Jeshi la Israel limeripoti Jumatatu kufanya mashambulizi ya usiku kucha dhidi ya majengo na eneo lilikuwa  linatumiwa na Hezbollah

Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Turk amesema Jumatatu kuwa kumaliza vita huko Gaza na kuepuka mzozo kamili wa kikanda ni kipaumbele cha haraka.

“Tunajua kwamba vita vinaenea, na katika vizazi vijavyo, na kukuza mzunguko wa mara kwa mara wa chuki kama sababu zao hazitashughulikiwa,” Turk alikiambia kikao cha Baraza la Haki za Binadamu mjini Geneva. “Cha kusikitisha, vita huko Gaza ni mfano muhimu”.

Turk alielezea shambulio la kutisha la Hamas dhidi ya Israel, lililowalazimisha kukosa makazi watu milioni 1.9 wa Gaza, Waisraeli 101 ambao bado wanashikiliwa mateka huko Gaza, na operesheni zilizopelekea vifo na uharibifu huko Ukingo wa Magharibi ambazo zinasababisha hali kuwa mbaya sana.

Jeshi la Israel limeripoti Jumatatu kufanya mashambulizi ya usiku kucha dhidi ya majengo na eneo lilikuwa linatumiwa na wanamgambo wa Hezbollah kusini mwa Lebanon, katika mapigano ya hivi karibuni ya mpakani kati ya pande hizo mbili ambayo yamezusha wasiwasi kuhusu mzozo mpana wa kikanda.