Vita ya maneno yazuka Sudan

Picha ya mwanamke na mtoto wake wakiwa wanasubiri chakula cha msaada kutoka WFP

Ni mzozo wa mafuta katika nchi za Sudan kusini na Kaskazini ambao sasa inabashiriwa unaweza kubadilika na kuwa vita

Sudan kusini na Sudan zimeingia katika vita vya maneno tangu kusini ilipositisha kusukuma mafuta kwenda kaskazini kutokana na mzozo wa bei. Pande zote mbili zimeonya kuwa uwezekano wa kurejea katika vita ni mkubwa.

Sudan kusini inaanda wanajeshi wake kufanya kazi kuimarisha jeshi la zamani la uasi la Southern People’s Rebelation Army kuwa jeshi rasmi.

Wanajeshi katika kituo cha kijeshi cha Bilpam huko Juba wanaweza kuitwa kuingia katika mapambano haraka kuliko ilivyotarajiwa, kama vita vya maneno dhidi ya mzozo wa mafuta huko Sudan vitabadilika na kuwa vitendo.

Sudan kusini ilisitisha upelekaji mafuta kupitia kaskazini ikidai kuwa nchi hiyo imeiba mamilioni ya dola ya mafuta ghafi. Khartoum inasema inachukua mafuta hayo kufidia gharama za usafirishaji ambazo hazijalipwa.

Naibu waziri wa ulinzi meja Majak D’ Agoot amesema hatua kama hizo ni tishio kubwa kwa taifa jipya.