Vita vya Israel dhidi ya Hamas vitadumu hadi mwisho wa mwaka; Tzachi Hanegbi

Mshauri wa usalama wa taifa wa Israel Tzachi Hanegbi

Tunaweza kuwa na miezi mingine saba ya mapigano ili kuimarisha mafanikio yetu na kuharibu nguvu za Hamas

Afisa wa ngazi ya juu wa Israel amesema anatarajia vita vya Israel dhidi ya Hamas katika Ukanda wa Gaza vitadumu hadi mwishoni mwa mwaka huu, licha ya wito unaoendelea kutolewa wa kusitisha mapigano.

“Tunaweza kuwa na miezi mingine saba ya mapigano ili kuimarisha mafanikio yetu na kufikia kile tulichokielezea kama kuharibu nguvu za Hamas na uwezo wa kijeshi,” mshauri wa usalama wa taifa Tzachi Hanegbi aliiambia redio ya umma ya Israeli siku ya Jumatano.

Wakati huo huo, waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, wakati wa ziara yake Moldova, alisema Israel inahitaji mpango wa baada ya vita “haraka iwezekanavyo” na kwamba kutokuwepo kwa mpango huo kunaweza kusababisha machafuko.

“Na nadhani hii inasisitiza umuhimu wa kuwa na mpango wa siku baada ya hapo, kwa sababu kukosekana kwa mpango wa siku baada ya hapo, hakutakuwa na mpango wa siku zijazo”, Blinken aliwaambia waandishi wa habari.

“Kama sivyo, Hamas itaachwa madarakani, jambo ambalo halikubaliki. Au kama sivyo, tutakuwa na machafuko, ukosefu wa sheria na mapigano”.