Vietnam imethibitisha kesi mbili za kwanza za maambukizo ya mbu wenye virusi vya Zika.
Wizara ya afya ya nchi hiyo imesema mapema leo kwamba mwanamke mwenye miaka 64 katika ufukwe maarufu ya Nha Trang, na mwanamke mwengine mwenye miaka 33 kutoka Ho Chi Minh waligundulika kuwa na virusi vya Zika mwishoni mwa mwezi Machi na wote walilazwa hospitalini wakiwa na homa, matatizo ya macho na vipele.
Chombo cha habari cha serikali kinasema mwanamke mwenye miaka 33 ni mjamzito. Wote wawili wanaelezwa kuwa katika hali nzuri. Kesi nyingi za Zika hazisababishi kuumwa sana na waathirika wengi hawaonyeshi dalili zozote.