Viongozi wa Ulaya wanaokutana Brussels wajadili kukabiliana na kushuka kwa uchumi

Rais wa Baraza la Ulaya Charles Michel akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumalizika siku ya kwanza ya kilele cha Mkutano wa Umoja wa Ulaya kumalizika huko Brussels Aprili 18, 2024.

Viongozi wa Ulaya wako katika siku ya pili ya mkutano hivi leo wa Baraza la EU mjini Brussels, ambapo mazungumzo hivi leo yanalenga jinsi ya kuondoa tatizo la kushuka kwa uchumi katika umoja huo na kuuzuia kuwa nyuma zaida ya China na Marekani.

Viongozi hao walisikiliza pendekezo la juhudi pana za EU katika kutoa ruzuku kwa makampuni ikiwa ni majibu kwa utawala wa Biden kuunga mkono uwekezaji katika teknolojia rafiki kwa mazingira.

Uwekezaji huu ni kupitia sheria ya Inflation Reduction, na pia kuhusu ruzuku ya China kwa magari ya umeme na panel za nguvu ya jua.

Charles Michel, Rais wa Baraza la Ulaya anasema: “Ushindani suala la msingi. Tunakabiliwa na changamoto mbali mbali, changamoto ya hali ya hewa, ya digitali, uharaka wa kuwekeza zaidi katika usalama na ulinzi, kuna masuala pia ya demografia.

Na kwa hili, kuna jibu, ni kuimarisha soko la ndani, kuboresha kanuni, kuendelea soko la nishati na kuendelea na kuweka mikakati ya uwekezaji. Hilo ndiyo liko hatarini.”

Mkuu wa EU Charles Michel amesema jana kuwa viongozi walikubaliana kuweka vikwazo vipya kwa uzalishaji wa Iran wa Drone na makombora kutokana na shambulizi la mwishoni mwa wiki la Tehran kwa Israel.