Viongozi wa mataifa 5 ya kiarabu kukutana Misri kujadili mzozo wa nishati na chakula

Rais wa Mistri Abdel Fattah al-Sisi akihudhuria mkutano kati ya Jumuia ya nchi za kiarabu na nchi wanachama wa Umoja wa ulaya, katika mji wa mapumziko wa Sharm el-Sheikh, Mistri, Februari 24, 2019. Picha ya Reuters

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi leo Jumanne atakuwa mwenyeji wa mkutano wa mataifa matano ya kiarabu, huku mizozo ya nishati na chakula inayohusiana na vita vya Ukraine ikiwa kwenye ajenda ya mkutano huo, serikali imesema

Sisi, Rais wa Umoja wa falme za kiarabu Bin Zayed Al-Nahyan, waziri mkuu wa Irak Mustafa al-Kadhemi na wafamle wa Jordan na Bahrain, Abdullah II na Hamad, wote pamoja, wanatarajiwa kufanya mkutano huo huko El-Alamein, kaskazini magharibi mwa Cairo kwenye pwani ya Mediterania.

Viongozi hao watano walikutana Jumatatu, ikulu ya Mistri imesema katika taarifa, na walijadili njia za kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi zao.

Hata hivyo, msemaji wa ikulu ya Mistri amesema mkutano rasmi unazinduliwa leo Jumanne, baada ya vyombo vya habari vya Misri kusema hapo awali kwamba ungeanza jana Jumatatu.

Kwa mujibu wa gazeti la serikali ya Misri Al-Ahram, mkutano huo utashughulikia masuala ya “nishati na usalama wa chakula”.