Viongozi wa mapinduzi nchini Niger ambao wanasema wamepindua serikali iliyochaguliwa walipata uungwaji mkono mkubwa wa jeshi na kutoa wito wa utulivu siku ya Alhamisi baada ya waandamanaji vijana kuvamia na kupora kwenye makao makuu ya chama tawala.
Mlengwa wa hivi karibuni zaidi wa mapinduzi katika eneo lenye machafuko la Sahel barani Afrika, Rais Mohamed Bazoum amezuiliwa katika makazi yake tangu Jumatano na walinzi wake .
Bazoum amekaidi mapinduzi hayo na kuonyesha msimamo wake wakati shutuma zikiongezeka kutoka mashirika ya kimataifa ya Afrika na kimataifa, na washirika Ufaransa, Ujerumani na Marekani.
Mafanikio hayo ya demokrasia yaliyopatikana kwa taabu yatalindwa, Bazoum alisema kwenye mtandao wa Twitter ambao unabadilishwa jina kuwa X.