Viongozi wa Afrika wanaelekea katika mji mkuu wa China wiki hii, wakitafuta ufadhili kwa ajili ya miradi mikubwa ya miundombinu wakati wakishuhudia ushindani mkubwa wa nguvu juu ya rasilimali na ushawishi katika bara hilo.
China imeongeza uhusiano wake na mataifa ya Afrika katika muongo mmoja uliopita, na kuwapatia mikopo ya mabilioni ambayo imesaidia kujenga miundombinu, lakini pia wakati mwingine ilizua utata kwa kuzitumbukiza nchi katika madeni makubwa.
China imepeleka maelfu ya wafanyakazi barani Afrika kujenga miradi yake mikubwa, wakati ikijiimarisha kwa rasilimali kubwa za bara hilo, ikiwemo shaba, dhahabu, Lithium na madini mengine adimu ya ardhini.
Beijing imesema mkutano wa wiki hii kati ya China na Afrika utakuwa tukio kubwa zaidi la kidiplomasia tangu janga la COVID-19, huku viongozi wa Afrika Kusini, Nigeria, Kenya na mataifa mengine yakithibitishwa kuhudhuria na wajumbe kadhaa wanatarajiwa kuwepo huko.