Viongozi wa Afrika Mashariki wakubaliana kuongeza muda wa kikosi cha Afrika mashariki nchini DRC

Wanajeshi wa Kenya wakihudhuria hafla iliyosimamiwa na rais wa Kenya William Ruto kabla ya kupelekwa nchini DRC kushiriki katika kikosi cha Afrika mashariki, Novemba 2, 2022.

Viongozi wa Afrika Mashariki Jumanne walikubaliana kuongeza muda wa kikosi cha Afrika Mashariki kilichopelekwa kukomesha ghasia katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Jumuiya ya Afrika Mashariki yenye nchi wanachama saba ilipeleka kwa mara ya kwanza wanajeshi katika eneo hilo lenye mzozo mwezi Novemba mwaka jana baada ya uasi wa kundi la M23 kuibuka tena.

Taarifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyotolewa jana Jumanne baada ya mkutano wa mjini Nairobi ilisema marais wa nchi wamekubaliana “kuongeza muda wa mamlaka” ya kikosi cha kikanda kinachojulikana kama EACRF hadi tarehe 8 Disemba, ikisubiriwa ripoti ya tathmini.

Mstakabali wa kupelekwa kwa wanajeshi hao ulikuwa mashakani baada ya Rais wa DRC Felix Tshisekedi kukikosoa kikosi hicho, lakini Jumuiya ya Afrika Mashariki iliamua mwezi Juni wanajeshi hao wabaki huko kwa miezi mingine mitatu.

Makundi mengi yenye silaha yanavuruga usalama katika eneo la mashariki mwa DRC lenye utajiri wa madini, ukiwa urithi wa vita vya kikanda ambavyo vilipamba moto katika miaka ya 1990 na