Viongozi mbalimbali wametuma ujumbe wao wakati Marekani inajitayarisha kwa utawala mpya chini ya Joe Biden.
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema bungeni kwamba ana matumaini makubwa ya ushirikiano mwema kutoka kwa utawala mpya wa Marekani, utakaoimarisha ukuaji wa Marekani na Uingereza, kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, vitisho vya kiusalama na kukabiliana na janga la virusi vya Corona.
Mkuu wa tume ya umoja wa ulaya Ursula Von Der Leyen, ameandika ujumbe wa twiter kwamba Marekani imerejea na umoja wa ulaya upo tayari kwa kurejea huko na kurejesha uhusiano mema, maisha mapya na ushirikiano wa kujivunia.
Nchini Ujerumani, rais Frank Walker Steinmeier, ametuma ujumbe wa video unaosema kwamba leo ni siku nzuri sana kwa demokrasia na kwamba ana furaha kubwa sana kwamba Joe Biden anaingia madarakani hii leo na kwamba ana Imani kuwa watu wengi nchini Ujerumani wana hisia nzuri sana.
Waziri mkuu wa Italy Giuseppe Conte ameelezea matumaini kwamba ushrikiano wa nchi 20 zenge nguvu zaidi duniani itaimarika wakati wa utawala wa Joe Biden huku msemaji wa serikali ya Russia Dmitry Peskov akisema kwamba Russia ipo tayari kulinda makubaliano kuhusu silaha.