Viongozi duniani wafuatilia uchaguzi wa Marekani

Wakati wamarekani wakiendelea kusubiri matokeo ya uchaguzi wa rais ulokua na ushindani mkali, viongozi wa dunia wameanza kutoa maoni yao juu ya matokeo hayo. Wakati huo huo wachambuzi wameanza kutafakari juu ya kwa nini utafiti wa maoni ya wapiga kura kwa mara nyingine tena umetoa utabiri tofauti na matokeo.

Kabla ya uchaguzi utafiti ulionesha mgombea wa chama cha demokratik Joe Biden atapata ushindi mkubwa katika majimbo yenye ushindani, lakini kufikia leo imedhihirika kuna ushindani mkubwa kati yake na Rais Donald Trump.

Kansela wa ujerumani Angela Merkel hii leo ametoa wito kwa kura zote kuhesabiwa katika uchaguzi huo ulokua na ushindani na kusisitiza kwamba marekani itaendelea kua mshirika muhimu wa ujerumani Pamoja umoja wa ulaya bila ya kujali matokeo yake.

Msimamo huo unmelezwa na viongozi wengi wa dunia hii leo wakati watu wakisubiri kwa hamu matokeo ya uchaguzi wa taifa kuu la kiuchumi duniani.

Hapa maekani kwa upande mwengine Wachambuzi wanasema huwenda inabidi kuwepo na mageuzi kamili juu ya namna utafiti unafanyika, kwa kuangalia kasoro na mapungufu yanayotokea. Katika uchauzi huu rais Trump amepata uungaji mkono mkunwa wa wapigaji kura wa maeneo ya mashambani huku Biden akipata uungaji mkono mkubwa kutoka maeneo ya mijini.

Gazeti la Wall Street Journal pia limeandika tahariri inayokosowa wataalamu wanaofanya utafiti wa maoni ya wananchi na wachambuzi, na kusema ushindi ulotabiriwa wa Biden haujashuhudiwa.

Matokeo hayo hivi sasa wanasema wadadisi yatasababisha watu kutoamini tena utafiti wa maoni kwani ni matokeo saw ana yale yaliyotolewa mwaka 2016 pale Hillary Clinton alionekana atapata ushindi lakini matokeo yake ni Trump aliyebuka mshindi.

Inaonekana utafiti haukuchukua maoni ya watu wngi wa mashambani walompatia ushindi mkubwa Trumo katika majimbo mengi Pamoja na maoni ya wakazi kutoka nchi za amerika kusini hasa wale wenye asili ya Cuba katika jimbo la Miami ambako walijitokeza kwa wingi kumpigia kura Trump.

Inavyonekana hivi sasa vita vya kutetea matokeo hayo vitatokea mahakamani kwani Trump ametangaza atawasilisha mashtaka kusitisha kuhesabiwa kura. Hilo linaonekana halitafanikiwa lakini kuna uwezekano akapinga matokeo kama ilivyotokea mwaka 2000 wakati wa ushindani kati ya George Bush na Al Gore.