Vikosi vya Ukraine bado vinashikilia mji wa Sievierodonetsk vikipambana na mashambulizi ya Russia

Magari ya kijeshi yakiwa katika mkoa wa Donetsk.

Vikosi vya Ukraine bado vinaushikilia mji wa Sievierodonetsk Jumanne  wakati vikipambana na mashambulizi ya Russia baada ya uvamizi wa Russia.

Vikosi vya Ukraine bado vinaushikilia mji wa Sievierodonetsk Jumanne wakati vikipambana na mashambulizi ya Russia baada ya uvamizi wa Russia.

Pande zote mbili zimesema vikosi vya Russia sasa vinadhibiti kati ya theluthi moja na nusu ya mji huo. Wawakilishi wa Russia wanaotaka kujitenga walikiri kwamba kukamatwa huko kulichukua muda mrefu kuliko ilivyotarajiwa licha ya moja ya mashambulio makubwa ya vita.

Wachambuzi wa kijeshi wa nchi za magharibi wanasema Moscow wamehamisha nguvu kazi na matumizi ya silaha kutoka maeneo mengine ili kuelekeza nguvu zaidi katika mji wa sievierodonetsk wakitarajia kwamba mashambulizi makubwa katika mji huo mdogo wa kibiashara yanaweza kusababisha kitu ambacho Russia inaweza kukiita ushindi katika mojawapo ya malengo yake yaliyotajwahuko mashariki.

“tunaweza kusema tayari kwamba theluthi moja ya Sievierodonetsk tayari iko chini ya udhibiti wetu, shirika la habari ya serikali ya Russia – TASS limemnukuu Leonid Pasechnik, kiongozi wa jamhuri ya Luhansk inayoiunga mkono Moscow, akisema .

Mapigano yalikuwa yakiendelea katika mji huo, lakini vikosi vya Russia havijasonga mbele kwa kasi kama ilivyotarajiwa, aliongeza kusema akidai kwamba vikosi vinavyoiunga mkono Moscow vinataka kutunza miundo mbinu ya mji huo na kufanya operesheni taratibu kwa sababu ya tahadhari karibu kwa kiwanda cha kemikali.

Vikwazo vipya vinavyotarajiwa kurasimishwa na viongozi wa umoja wa ulaya leo vitazuia asilimia 75 ya uagizaji wa mafuta ghafi ya Russia. Hii itaongezeka hadi asilimia 90 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.