Idadi hiyo imelinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita wa 2020.IOM limesema kuwa lina wasi wasi kutokana na ongezeko la vifo kwenye njia hatari baharini inayotumiwa na wahamiaji kutoka Afrika wakati wakelekea Ulaya.
Shirika hilo Jumatano limesema kwamba takriban watu 1,146 wamekufa wakati wakijaribu kuvuka kwelekea Ulaya katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Wengi wa waliokufa wanasemekana kuwa kwenye bahari ya Mediterranean.
Idadi ya wahamiaji wanaojaribu kuvuka pia imeongezeka wakati zaidi ya watu 31,500 wakikamatwa, au kuokolewa na serikali za kaskazini mwa Afrika katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, wakilinganishwa na takriban 23,000 mwaka uliopita kwenye kipindi sawa na hicho.
Wengi wa wahamiaji wanasemekana kutokea Tunisia wakielekea Italy. Italy imetajwa kuwa na wasi wasi mkubwa kutokana na ongezeko hilo kama alivyosema waziri wake wa mambo ya kigeni Luciana Lamorgese wakati akifanya mahojinao na televisheni moja ya Italy.