Idadi ya vifo kufuatia mlipuko wa lori la mafuta karibu na mji mkuu wa Uganda Kampala wiki iliyopita imeongezeka na kufikia 24, serikali imesema leo Jumapili.
Nchi hiyo maskini ya Afrika Mashariki imeshuhudia majanga kadhaa kama hayo katika miaka ya hivi karibuni, huku watu wakikimbilia kuiba mafuta kutoka kwenye malori ya mafuta yaliyopata ajali barabarani.
“Ajali mbaya iliyotokea Jumanne katika mji wa Kigogwa, takriban kilomita 25 kaskazini mwa Kampala, iliripotiwa kuwa watu 11 walifariki katika eneo la tukio”, alisema Waziri wa Mawasiliano Godfrey Kabbyanga katika taarifa yake.
Aliongeza kuwa watu wengine 13 wamefariki dunia katika hospitali ya Kiruddu na hospitali ya jeshi ya Bombo na kufikisha idadi ya vifo 24”. Kwa kuwa baadhi ya waliofariki waliungua sana na moto na kushindwa kutambuliwa, polisi wamekuwa jitihada kubwa kumtambua kila marehemu kupitia uchunguzi wa DNA, alisema.