Vifaru wanne weupe wamekufa nchini Zimbabwe baada ya kunywa maji kutoka katika ziwa lililochafuliwa na maji taka ambalo pia ndilo msambazaji mkuu wa maji karibu na mji mkuu
Vifaru wanne weupe wamekufa nchini Zimbabwe baada ya kunywa maji kutoka katika ziwa lililochafuliwa na maji taka ambalo pia ndilo msambazaji mkuu wa maji karibu na mji mkuu, mamlaka ya wanyamapori ilisema leo Jumamosi.
Pundamilia watatu, nyumbu wanne, tai wanne pamoja na mbuzi na ng'ombe kadhaa pia walikufa wiki iliyopita baada ya kunywa maji kutoka Ziwa Chivero lililopo kilometa 30 kutoka Harare, msemaji aliiambia AFP.
Wanyama hao wamepata sumu na cyano-bacteria ambayo pia ni sumu kwa binadamu.
Taasisi ya ZimParks iliwahamisha vifaru waliosalia kutoka Hifadhi ya Ziwa Chivero ili kuepusha vifo zaidi, alisema.