Venezuela ilisema Jumamosi itasitisha mashauriano na upinzani ambayo yalipangwa kuanza tena Jumapili baada ya Cape Verde, kumkabidhi mfanyabiashara wa Colombia, Alex Saab, mwakilishi wa Venezuela kwa Marekani kwa tuhuma za biashara haramu ya fedha.
Tangazo hilo lilitolewa na mbunge wa chama cha Socialist, Jorge Rodriguez, ambaye anaongoza timu ya mashauriano ya serikali. Rodriquez alisema serikali ya Venezuela haitahudhuria mazungumzo yatakayoanza leo Jumapili.
Serikali ya Venezuela hapo Septemba ilimtaja Saab, ambaye alikamatwa Juni mwaka 2020 wakati ndege yake iliposimama Cape Verde ili kuongeza mafuta, kama mshiriki wa timu ya mazungumzo na upinzani huko Mexico, ambapo pande hizo mbili zinatafuta njia ya kutatua mzozo wao wa kisiasa.