Venezuela yakamata wanahabari

Serikali ya Venezuela imewakamata wanahabari tisa na kuwafukuza 14  kuondoka nchini humo kabla na mara baada ya uchaguzi wenye utata.

Watano kati ya hao walikamatwa wiki iliyopita, huku serekali ikiwashutumu waandishi wa habari kwa mashtaka yanayohusiana na ugaidi.

Wafanyakazi wa vyombo vya habari pia wametishwa, kujeruhiwa na kufukuzwa, kwa mujibu taarifa kutoka kwa vyama vya vyombo vya habari na vikundi vya uhuru wa kujieleza.

Katika tukio baya zaidi, mwandishi wa habari alipigwa risasi na kujeruhiwa katika jimbo la Aragua.

Kwingineko, wasemaji wa serikali za kitaifa na serikali za mitaa wanaripotiwa kuwanyanyasa wanahabari.

Taasisi ya vyombo vya habari na jamii (IPYS), imeandika takeiban ukiukwaji 79 wa uhuru wa vyombo vya habari kati ya Julai 29, siku moja baada ya uchaguzi na Agosti 4 umefanyika.

Kesi nyingi zinahusishwa na habari za uchaguzi au maandamano.