Jumanne Vatican inasema Papa Francis amekunywa chai na kusoma magazeti na kutembea wakati anaendelea kupona kutokana na upasuaji wa tumbo. Taarifa kutoka kwa msemaji wa Vatikani, Matteo Bruni, ilisema vipimo vilivyofanywa kufuatia upasuaji wa papa huyo Jumapili kuondoa nusu ya utumbo wake mpana ulitoa matokeo mazuri na ya kawaida.
Bruni alisema Jumanne kwamba Francis alipumzika vizuri usiku kucha. Papa mwenye umri wa miaka 84 alifanyiwa upasuaji kwa masaa matatu kwa kile ambacho Vatican ilisema ni kupungua nafasi ndani ya utumbo mkubwa. Vatican ilisema madaktari waliondoa upande wa kushoto wa utumbo wake mpana.
Anatarajiwa kukaa katika hospitali ya Roma na kwenye chumba maalum kilichotengwa kwa mapapa kwa wiki,wakiwa na matumaini hakutakuwa na shida yoyote.