Uturuki yawakamata watu 29 wanaoshukiwa kuwa na mafungamano na Islamic State

Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan of Turkey

Kufuatia vyanzo vya usalama shirika la habari la uturuki Anadolu limesema kwamba watuhumiwa wengine watatu wanaohusishwa na 29 walioshikiliwa wamekamatwa katika operesheni hiyo pia. Imesema watatu hao walikuwa wanachama wa juu wa kundi la Islamic state , na kuongeza kuwa mmoja alipanga shambulizi katika ubalozi wa Iraq mjini Ankara.

Watuhumiwa walikamatwa katika operesheni zinazojulikana kama “ heroes 37” zilizofanyika ijumaa ambapo taarifa zilikusanywa katika makanisa na mahekalu mjini instanbul , alisema hayo Yerlikaya katika mtandao wa kijamii wa X akiongeza kuwa maeneo mengine 39 yalivamiwa.

Maafisa walianzisha operesheni dhidi ya wanamgambo wa Islamic state na wa Kikurdi baada ya wanamgambo wa Kikurdi kulipua bomu karibu na majengo ya serikali mjini Ankara Octoba Mosi.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali