Lira ya Uturuki imepoteza thamani dhid ya dola kwa kiasi cha asilimia 20 tangu mwaka huu kuanza na kuongeza hofu ya kuongezeka kwa bei ya bidhaa hasa chakula.
Uturuki imekumbana na ukosefu mkubwa wa pesa, na mfumuko wa bei tangu mwaka 2021
Wataalam wa uchumi wanaamini kwamba hali hiyo imesababishwa na fikra za Erdogan kwamba kuongeza kiwango cha riba ni hatua itakayopelekea kuongezeka kwa mfumuko wa bei.
Erdogan ameshinkiza benki kuu ya Uturuki kupunguza gharama ya kupata mikopo, kinyume na hatua zingine zinazochukuliwa na benki zingine kuu duniani za kuongeza gharama ili kudhibithi bei.
Benki kuu ya Uturuki imepunguza kiwango cha riba kutoka asilimia 19 mwaka 2021 hadi asilimia 8.5 lakini mfumuko wa bei ulipanda hadi asilimia 85 mwaka uliopita.