Utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump umewafuta kazi wajumbe waliobaki wa baraza la ushauri kwa rais juu ya HIV na Ukimwi inayojulikana kama PACHA.
Wajumbe wa kamati hiyo walipokea barua wiki hii ikieleza kwamba uteuzi wao kwenye jopo hilo ulisitishwa mara moja kwa mujibu wa ripoti katika gazeti la The Washington Post. PACHA ilianzishwa mwaka 1995 wakati wa utawala wa rais wa zamani wa Marekani Bill Clinton ili kutoa ushauri kwa Ikulu ya Marekani-White House juu ya mikakati na sera za HIV.
Wajumbe sita wa baraza hilo wamechukizwa na hatua ya White House juu ya sera za afya na walijiuzulu mwezi Juni. Scott Schoettes mwanasheria wa Lambda Legal, taasisi ya haki za mashoga-LGBT alikuwa mmojawao. Aliandika katika gazeti la Newsweek kuwa katika kipindi ambacho Rais wa Marekani Donald Trump hajali kuhusu watu wanaoishi na HIV.
Schoettes alisema utawala wa Trump unashinikiza usajili ambao unawaumiza watu wanaoishi na HIV na kuumiza au kugeuza hatua muhimu iliyofikiwa katika mapambano dhidi ya ugonjwa huu.