Utawala wa Obama uko tayari kusaidia Nigeria

Utawala wa Obama uko tayari kusaidia Nigeria

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hillary Clinton amesema utawala wa Obama uko tayari kuisaidia Nigeria katika njia yoyote iwezekanayo kufanya uchaguzi ujao kuwa wa huru na haki.

Clinton alitoa rai hiyo jana hapa Washington kufuatia mkutano na waziri wa mambo ya nje wa Nigeria Henry Odein Ajumogobia.

Alisema mazungumzo hayo yalilenga kwenye muda mdogo uliopo kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi wa rais na wabunge mwezi January.