Maafisa wa usalama Marekani wanasema wanachukua kila tahadhari kujilinda dhidi ya shambulizi lolote siku ya Jumatano wakati wa kuapishwa kwa Rais mteule Joe Biden, nje ya jengo la bunge la Marekani ikiwemo uchunguzi wa usalama unaofanywa na FBI dhidi ya walinzi wa taifa 25,000 waliopangiwa kulinda sherehe hiyo Washington.
Kaimu waziri wa ulinzi Christopher Miller anasema katika taarifa yake kwamba “ingawa hatuna taarifa ya ujasusi inayoonesha tishio la ndani, hatutaacha kuchukua hatua yeyote ya ziada katika kuulinda mji mkuu”.
Wakati huo huo ripoti za ujasusi Marekani zinaeleza kwamba baadhi ya waandamanaji bado wanaamini kuwa Rais Donald Trump anayemaliza muda wake madarakani aliibiwa kura katika uchaguzi wa marudio, na huwenda akajaribu kuvuruga sherehe za kuapishwa kwa Biden hapo Januari 20.
Eneo litakapofanyika sherehe za kuapishwa limezungushiwa uzio mrefu wa chuma, usalama umeongezwa zaidi kuliko ilivyo kawaida katika sherehe zilizofanyika miaka minne iliyopita.