Upinzani waongoza kwenye uchaguzi wa Lithuania

  • VOA News

Kiongozi wa chama cha Social Democrats, Vilija Blinkeviciute, akizungumza na wanahabari baada ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa bunge wa Lithuania. Oct. 13, 2024.

Chama cha upinzani cha Lithuania cha Social Democrats, kilionekana kuongoza kwenye kura ya pili ya bunge Jumapili, wakati wapiga kura wakiashiria kuwa na wasi wasi kutokana na kupanda kwa gharama ya maisha, pamoja na tishio la kiusalama kutoka kwa Russia ambaye ni jirani.

Takwimu rasmi za serikali zimeonyesha chama hicho chenye msimamo wa kati kushoto kikiongoza kwa viti 33 baada ya kuhesabiwa kwa asilimia 64 ya kura, kando na viti 20 kilichopata kwenye duru ya kwanza ya uchaguzi, katika bunge hilo lenye jumla ya viti 141.

Chama tawala cha Homeland Union Party, kilipata viti 6 kando na zile 18 kilichopata kwenye duru ya kwanza. Taifa hilo la Baltic lenye jumla ya wakazi milioni 2.9 kina mfumo wa upigaji kura ambapo nusu ya viti vya bunge huchaguliwa kupitia wingi wa kura, huku vilivyobaki vikiwa ni kupitia uchaguzi wa marudio kwenye wilala kati ya wagombea wawili wanaoongoza, na mara nyingi hunufaisha vyama vikubwa.

Iwapo chama cha Social Democrats kitafaulu kuunda serikali, basi kinatarajiwa kuendeleza msimamo wa Lithuania dhidi ya Russia, pamoja na utumizi mkubwa wa fedha za ulinzi. Tiafa hilo mwaka huu litatumia takriban asilimia 3 ya mapato yake ya ndani kwenye jeshi, kulingana na makadirio ya NATO, na kwa hivyo kulifanya kuwa taifa la 6 mwanachama ifikapo kwenye matumizi ya kiusalama.