Upinzani huko Chad umeahirisha maandamano ya Ijumaa

Polisi wa Chad wakiwa ofisi za makao makuu ya upinzani huko Ndjamena

Asasi za kiraia na chama cha Transformers cha mpinzani Succes Masra walitaka kufanya maandamano huko N'Djamena dhidi ya ukiukaji wa kimfumo wa  haki za binadamu na kutwaa madaraka kwa baraza la kijeshi la mpito

Upinzani mkuu nchini Chad, ambao ulikuwa umeidhinishwa kwa mara ya kwanza kuandamana siku ya Ijumaa dhidi ya utawala wa kijeshi umeamua kuahirisha uhamasishaji kwa sababu ya kutokubaliana juu ya njia iliyotangazwa kwa mujibu wa AFP.

Asasi za kiraia na chama cha Transformers cha mpinzani Succes Masra walitaka kufanya maandamano huko N'Djamena dhidi ya ukiukaji wa kimfumo wa haki za binadamu na kutwaa madaraka kwa baraza la kijeshi la mpito . Maandamano hayo yameahirishwa hadi tarehe nyingine mratibu wa maandamano aliliambia shirika la habari la AFP.

Wanaharakati hao walitaka maandamano yafanyike Jumatano, lakini Waziri wa Usalama wa Umma, Souleymane Abakar Adoum alitoa ruhusa ya kuandamana Ijumaa akieleza kwamba ikitokea kosa au jambo lolote waandaaji watawajibika.

Maandamano hayo yaliidhinishwa kupita kwenye barabara yenye urefu wa kilomita 3 katikati mwa mji mkuu wa Chad.