Upigaji kura unaendelea Georgia

Bendera za Georgia, Umoja wa ulaya na Ukraine kwenye kituo cha kupigia kura Tbilisi, Georgia, Jumamosi Oct 26 2024 Picha: AP

Wapiga kura nchini Georgia leo Jumamosi wameshiriki katika zoezi la upigaji kura ambapo uchaguzi utakaoamua hali ya demokrasia Ulaya, wakati wasi wasi ukiongezeka kuhusu mwelekeo wa chama tawala kuelemea upande wa Russia.

Uchaguzi wa bunge unawahusisha wanasiasa wa upinzani wanaoyaunga mkon mataifa ya magharibi dhidi ya chama tawala cha Georgian Dream ambacho kinashutumiwa kukandamiza demokrasia na kuiunga mkono Russia.

Ukusanyaji maoni katika nchi yenye takriban watu milioni nne unaashiria kuwa vyama vya upinzani vinaweza kupata kura za kutosha kuunda serikali ya muungano itakayoongozwa na bilionea Bidzina Ivanishvili.

Mwanasiasa anayeegemea upande wa magharibi Salome Zurabishvili, amesema kwamba uchaguzi huo utaamua hali ya baadaye ya Georgia.