Wakati wanajeshi wakiendelea kuonekana, Ujumbe huo una wasiwasi mkubwa kwamba maendeleo haya ya hivi karibuni katika sehemu ya kusini ya Abyei yatazidisha mzozo katika eneo hilo na kusababisha mateso yasiyoelezeka na wasiwasi wa kibinadamu kwa raia katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa ujumbe huo ulibainisha kuwa Boksi la Abyei unasalia kuwa eneo lisilo na silaha ambalo halipaswi kuwa na nguvu yoyote iwe ya kawaida au yenye silaha ya jumuiya zote mbili. Kwa hivyo ni muhimu kwamba wote waheshimu maazimio husika ya Baraza la Usalama katika suala hili.
UNISFA ililaani mapigano mapya ndani na nje ya mipaka ya eneo hilo na kuzitaka pande zote kusitisha mapigano na kuruhusu mchakato wa kisiasa kusuluhisha mzozo unaoendelea. Wanasisitiza kuwa ni kinyume cha aina yoyote ya upelekaji wowote wa wanajeshi usioidhinishwa ndani ya eneo hilo.