UNICEF yasema watoto milioni 40 Duniani wameshindwa kusoma chekechea kutokana na Corona

UNICEF ni shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya watoto

Mkanganyiko wa elimu uliosababishwa na janga la COVID-19 unawazuia watoto kuanza kupata elimu yao wanayostahili ilisema taarifa ya UNICEF

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia masuala ya Watoto-UNICEF lilisema Jumanne kwamba kufungwa kwa majengo ya elimu kutokana na janga la COVID-19 limepelekea watoto milioni 40 wa shule za chekechea Duniani kukosa kusoma na kupata maendeleo.

Mkanganyiko wa elimu uliosababishwa na janga la COVID-19 unawazuia watoto kuanza kupata elimu yao wanayostahili, alisema mkurugenzi mtendaji wa UNICEF, Henrietta Fore katika taarifa yake.

Huduma ya mtoto na elimu ya awali kwa mtoto inajenga msingi bora ambao kila mtoto anategemea kupata maendeleo hayo. Janga la COVID-19 limeweka msingi wa elimu kuwa kwenye kitisho kikubwa. Utafiti mfupi ulioelezewa na ofisi ya utafiti ya UNICEF ulilenga kwenye hali ya elimu inayotolewa awali kwa mtoto na huduma ya mtoto pamoja na madhara ya janga la Corona yanavyowaathiri.