Kamishna mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la wakimbizi (UNHCR) ameonya kwamba kusuasua kwa misaada kunaongezeka wakati ambapo idadi kubwa ya watu wanakimbia migogoro, mateso, ukiukwaji wa haki za binadamu, mabadiliko ya hali ya hewa na umaskini mkubwa.
“Migogoro imesababisha watu wengi kuyahama makazi yao kwa idadi kubwa.
Wakimbizi milioni 110 na waliohama makazi yao ni idadi kubwa zaidi katika miongo kadhaa,” Filippo Grandi, mkuu wa UNHCR, alisema alipofungua mkutano wa kila mwaka wa shirika hilo.
Tukio hilo la kila mwaka lilianza dakika moja ya ukimya kukumbuka walio poteza maisha katika tetemeko la ardhi la hivi karibuni nchini Afghanistan na shambulizi la Israeli, matukio mawili ambayo yalikumba nchi hizo mbili siku ya Jumamosi na athari mbaya kwa mamilioni wengine.