Taarifa hiyo imetolewa muda mfupi baada ya Umoja huo kutoa ripoti nyingine mwezi uliopita ikionya kwamba taifa hilo changa zaidi duniani huenda likatumbukia tena kwenye mapigano, wakati ghasia za kikabila pamoja na migogoro ya kisiasa zikiendelea kuongezeka.
Kulingana na ripoti ya pamoja ya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, UNMISS, na ofisi ya haki ya kibinadamu, ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu pamoja na mauaji unafanyika katika wilaya ya Tambura katika jimbo la Western Equatoria,.
Ripoti hiyo inawalaumu kwa pamoja wanajeshi watiifu kwa rais Salva Kiir na wapiganaji wa kundi la SPLM/A-IO wanao ongozwa na makamu wa rais Riek Machar pamoja na washirika wa pande zote mbili. Ripoti inaeleza kwamba mbali na rais 440 walouliwa kati ya June na Septemba mwaka jana katika wilaya ya Tambura kuna visa 64 vya ubakaji vilivyoripotiwa na watu 74 kutekwa nyara.