UN yaisihi Uganda kurekebisha mswaada wa kupiga marufuku mahusiano ya jinsia moja

Raia wa Uganda wakishiriki kwenye matembezi ya kila mwaka ya wapenzi wa jinsia moja huko London, June 29, 2013.

Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa inatoa wito kwa Uganda kurekebisha mswaada wa kupiga marufuku mahusiano ya jinsia moja ambayo inasema yatakiuka viwango vya haki za binadamu na kudhoofisha afya ya umma.

Mswaada uliopitishwa na Bunge la Uganda wiki iliyopita, lakini bado haujakamilishwa umekuwa ukiandaliwa tangu mwaka 2015 na kupitia mabadiliko kadhaa muhimu. Maafisa wa haki za binadamu wanasema wanasikitishwa sana na uandikishaji na hatua hii ya hivi karibuni, ambayo italifanya kundi hili la watu kuwa wahalifu. Chini ya mswaada huo, wanaona uhusiano wa jinsia moja ungeadhibiwa vikali, kama vile wafanyabiashara ya ngono na wale walioambukizwa VVU.

Msemaji wa kamishna mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rupert Colville, anasema adhabu ya mswaada huo kwa mahusiano ya jinsia moja umepunguzwa hadi miaka 10 jela badala ya kifungo cha maisha. Walakini, anasema Sheria ya Makosa ya Kijinsia inaibua wasiwasi.

Colville amesema vifungu vingine vya kutisha katika Sheria hiyo ni pamoja na upimaji wa lazima na wa kulazimishwa wa VVU kwa washtakiwa.
UNAIDS, Mpango wa Pamoja wa Umoja wa Mataifa juu ya VVU / UKIMWI, inasema inaogopa suala la kuwakandamiza watu walioambukizwa VVU kutaondoa maendeleo mengi ambayo Uganda imepata katika kupunguza athari za ugonjwa huo. Tangu 2010, inasema, vifo vinavyohusiana na UKIMWI vimepungua kwa asilimia 60 na maambukizo mapya ya VVU yamepungua kwa asilimia 43.

Colville ameongeza kuwa mswaada huo unatoa ulinzi unaohitajika sana juu ya unyanyasaji wa kijinsia, jambo ambalo vikundi vya wanawake na vikundi vya kupambana na unyanyasaji wa kijinsia vimetetea kwa muda. Walakini, anasema muswada huo kwa ujumla, hauzingatii sheria na viwango vya kimataifa, na lazima urekebishwe.