UN inatoa wito kwa Sri Lanka kuhakikisha haki inatendeka kwa waathirika

Nembo ya Umoja wa Mataifa kitengo kinachohusika na haki za binadamu

Mjumbe wa ngazi ya juu wa UN, alitoa wito wakati Sri Lanka ikiadhimisha kumbukumbu ya waathirika  279 wa shambulio baya kuwahi kutokea

Umoja wa Mataifa umeitaka Sri Lanka kuondoa mwanya wake katika mapungufu ya uwajibikaji na kuhakikisha haki inatendeka wakati nchi hiyo ikiadhimisha kumbukumbu ya waathirika 279 wa shambulio baya zaidi kuwahi kutokea dhidi ya raia miaka mitano iliyopita.

Mjumbe wa ngazi ya juu wa Umoja wa Mataifa kwa nchi hiyo, Marc-Andre Franche, alisema katika ibada ya kumbukumbu mjini Colombo kwamba kuna haja ya kufanyika uchunguzi wa kina, na wa wazi ili kuwafichua wale waliohusika na mauaji ya Pasaka mwaka 2019.

Washambuliaji wa Kiislamu walishambulia makanisa matatu na hoteli tatu katika shambulizi la kujitoa mhanga lililowalenga raia, lakini familia zenye zinazoomboleza zinasema bado zinasubiri haki.

Miongoni mwa waliouawa ni raia 45 wa kigeni wakiwemo watalii wanaotembelea kisiwa hicho, muongo mmoja baada ya kumalizika kwa mzozo wa kikabila uliosababisha vifo vya zaidi ya watu 100,000 tangu mwaka 1972.