Mjumbe wa Sudan amepongeza hatua hiyo lakini amelitaka baraza hilo kuchukua hatua zaidi na kulichukulia vikwazo kundi la wanamgambo la Rapid Support Forces (RSF), kundi hasimu la jeshi la serikali ya Sudan.
“Kundi la wanamgambo kwa ujumla wake, hakika lazima liorodheshwe, sababu limekidhi masharti yote,” Balozi Al-Harith Idriss al Harith Mohamed alisema.
RSF imeteka eneo kubwa la Darfur, na vita vimekuwa vikiendelea tangu mwezi Mei katika mji mkuu wa Darfur Kaskazini, El Fasher, mji pekee wa jimbo la Darfur uliotekwa na RSF.
Jeshi la Sudan limeshtumu mara kadhaa Umoja wa Falme za Kiarabu kwa kutoa silaha na zana nyingine kwa RSF kupitia nchi jirani ya Chad. Umoja wa Falme za Kiarabu umekanusha vikali tuhuma hizo.