Mkuu wa kisiasa wa Umoja wa Mataifa alionya siku ya Jumatano kwamba Libya inaweza kuwa tena na tawala mbili zinazohasimiana na kurejea katika hali ya kutokuwa na utulivu, akitaka uchaguzi ufanyike haraka iwezekanavyo ili kuunganisha taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa mafuta la Kaskazini mwa Afrika
Naibu Katibu Mkuu, Rosemary DiCarlo ameliambia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba anatiwa moyo na kuungwa mkono kwa mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuitisha kamati ya pamoja kutoka Baraza la Wawakilishi la Libya na Baraza la Juu la Jimbo kwa lengo la kufikia makubaliano na vyombo vyote viwili kwa misingi ya kikatiba ambayo kuelekea uchaguzi mwaka huu.
Mgogoro huo ulianza baada ya Libya kushindwa kufanya uchaguzi wake wa kwanza wa rais Desemba 24 chini ya juhudi za upatanisho zinazoongozwa na Umoja wa Mataifa.