Umoja wa Mataifa ulisema siku ya Alhamisi kwamba maelfu zaid ya vifo katika janga la mafuriko nchini Libya vingeweza kuepukika ikiwa onyo la mapema na mifumo ya usimamizi wa dharura ungefanya kazi ipasavyo.
Kwa uratibu bora wa utendaji katika nchi iliyokumbwa na mzozo, wangeweza kutoa maonyo na vikosi vya usimamizi wa dharura vingeweza kutekeleza uhamishaji wa watu, na tungeweza kuzuia vifo vingi, Petteri Taalas mkuu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani la Umoja wa Mataifa, aliwaambia wanahabari mjini Geneva.
Maoni yake yalikuja baada ya mafuriko makubwa yenye ukubwa wa tsunami kupiga mashariki mwa Libya mwishoni mwa juma, na kuua takriban watu 4,000, huku maelfu wengine wakipotea na kuhofiwa kufariki dunia