Kwa mujibu wa msemaji wa Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Stephane Dujarric walipewa taarifa kwamba mikoa ya Kusini na Mashariki mwa Ethiopia inaendelea kukumbwa na athari za ukame mbaya ambao waliuzungumzia kidogo.
Baadhi ya maeneo hayo yanaendelea kukabiliwa na mlipuko wa kipindupindu, huku visa 1,100 vimerekodiwa hadi sasa.
Katika wiki za hivi karibuni, maelfu ya watu wamekimbia ghasia huko Somaliland hadi mkoa wa Somali.
Huko Kaskazini mwa Ethiopia, amesema ufikiaji wa misaada ya kibinadamu unaendelea kuboreka, kufuatia makubaliano ya kukomesha Uhasama. Ingawa maeneo machache yamesalia kuwa magumu kufikiwa, wao pamoja na washirika wa NGO na Serikali, wamepeleka zaidi ya malori 4,400 ya bidhaa za msaada katika mkoa wa Tigray tangu katikati ya Novemba, ikibeba karibu tani 180,000 za chakula na vifaa vingine vya misaada.
Lakini msaada huu unahitaji kuendelezwa. Zaidi ya watu milioni 8.5 kwa sasa wanalengwa kwa msaada wa chakula kote Afar, Amhara na Tigray.