Umoja wa Afrika umekuwa mwanachama rasmi  wa kudumu wa G20

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi, kulia, akimpokea Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika na Rais wa Muungano wa Comoro Azali Assoumani alipowasili katika kituo cha mikutano cha Bharat Mandapam kwa ajili ya Mkutano wa G20 mjini New Delhi, India, Jumamosi, Septemba 9, 2023. AP

Umoja wa Afrika wenye  nchi wanachama 55, sasa una hadhi sawa na Umoja wa Ulaya taasisi pekee ya  kikanda yenye uanachama kamili.

Umoja wa Afrika umekuwa mwanachama rasmi wa kudumu wa G20, kundi linalojumuisha nchi tajiri na zenye nguvu duniani, Waziri Mkuu wa India Narendra Modi alisema katika mkutano wa umoja huo mjini New Delhi leo Jumamosi.

Umoja wa Afrika wenye nchi wanachama 55, sasa una hadhi sawa na Umoja wa Ulaya taasisi pekee ya kikanda yenye uanachama kamili. Ushiriki wake wa awali ulikuwa taasisi ya kimataifa ililiyoalikwa tu.

Modi katika hotuba yake ya ufunguzi katika mkutano huo aliialika AU, ambayo imewakilishwa na Mwenyekiti wake Azali Assoumani kuchukua kiti katika meza ya viongozi wa G20 kama mwanachama wa kudumu.

“Nina heshima kuikaribisha Umoja wa Afrika kama mwanachama wa kudumu wa Familia ya G20. Hii itaiimarisha G20 na pia kuimarisha sauti ya Global South”, ulisema ujumbe wake kwenye akaunti rasmi ya Modi kwenye mtandao wa kijamii wa X, ambao zamani ulijulikana kama Twitter.