Dunia yakaribisha mwaka wa 2018

Watu waliokusanyika mjini Quezon, Ufilipino, kuukaribisha mwaka mpya wa 2018. Jan 1, 2018.

Maeneo mbalimbali duniani kote yaliukaribisha mwaka mpya baadhi yakifanya hivyo siku ya Jumapili na mengine Jumatatu.  Wakazi na wageni kote bara Asia waliukaribisha mwaka huu wa 2018 kwa fataki na sherehe.

Maelfu ya watu katika miji mikubwa barani Afrika walikusanyika, na kusherehekea mwaka mpya kwa njia mabalimbali.

Vyombo vya habari viliripoti kwamba miji mikubwa nchini Kenya, Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na DRC ni baadhi ya sehemu ambako wakazi walikusanyika kwa sherehe za mwaka mpya.

Kwingineko, maelfu walikusanuyika katika bandari ya Victoria, mjini Hong Kong, kutazama dakika kumi za maonyesho ya muziki na fataki, zilizorushwa kutoka paa za nyumba.

Baadhi ya waliojitokeza kuukaribisha mwaka mpya mjini New York. Dec. 31, 2018.

New Zealand, Australia na visiwa vya Pacific, yalikuwa maeneo ya kwamnza kuukaribisha mwaka mpya.

Eneo la Mashariki mwa Marekani lilisherehekea ujio wa mwaka mpya zilipogonga saa sita usiku kwa shangwe na vigelegele katika miji mbalimbali.

Maafisa mjini New York, walikuwa wametangaza kuwa waliongeza ulinzi wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka mpya.

Inakadiriwa takriban watu milioni mbili walikusanyika kwenye eneo la Times Square kushuhudia sherehe hizo za kufana.

Saa moja baadaye, hafla zingine kubwa za kuukaribisha mwaka mpya pia zilifanyika mjini New Orleans, Louisiana, kati ya maeneo mengine ya Marekani ya Kati.

Baadaye majimbo yaliyo Magharibi mwa Marekani pia yakliukaribisha mwaka saa mbili baadaye. Hii ni kutokana na tofauti ya saa katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu.