Utafiti ambao umefanyika kwa mara ya kwanza ulimwenguni ukiangalia jinsi teknolojia ya kisasa inavyotumiwa na vyombo vya habari umebainisha mapungufu hayo.
Matokeo yaliyowasilishwa kutokana na utafiti kuhusu hali ya teknolojia katika vyumba vya habari ulimwenguni iliyofanywa na Kituo cha International Center for Journalists (ICFJ) umeonyesha ni maeneo gani ya dunia yanayoongoza na yaliyoko nyuma katika matumizi ya teknolojia ya kidigitali, pamoja na mambo mengine.
Wakati matatizo katika vyumba vya habari katika zama hizi yamefanyiwa tathmini, utafiti huo umejikita katika kile kinachokosekana: jinsi gani waandishi wa habari ulimwenguni wanavyotumia teknolojia.
Tafiti hii imetokana na majibu kutoka kwa zaidi ya mameneja wa vyumba vya habari 2,700 na waandishi wa habari kutoka nchi 130, waliowasilisha majibu yao katika lugha 12.
“Pamoja na mafanikio katika matumizi ya teknolojia, waandishi wa habari kwa uchache hawawezi kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko ambayo yanaikabili sekta hiyo,” amesema Joyce Barnathan, rais wa ICFJ.
“Utafiti huo pia unaainisha mapungufu, na kutuwezesha kufahamu vipi tunaweza kupiga hatua hivi sasa kuanzia mafunzo katika vyumba vya habari mpaka usalama wa kidigitali.”
Taasisi zilizosaidia katika tafiti hii, ni Storyful, Google News Lab na SurveyMonkey zilisaidi. Taasisi nyingine zilizoongoza tafiti hii na kuichambua ambayo iliwezeshwa kupitia mfumo wa SurveyMonkey Georgetown University’s Communication, Culture, na Technology program.
Matokeo ya tafiti hii yalikusanywa kutoka maeneo manane ya dunia: Eurasia/ na iliyokuwa USSR, Ulaya, Latin Amerika, Mashariki ya Kati/ Afrika Kaskazini, Amerika ya Kaskazini, Kusini mwa jangwa la Sahara-Afrika, Asia Kusini, na Mashariki/Kusini mashariki mwa Asia.