Ulaya yajitafakari baada ya ushindi wa Trump

Washirika wa Marekani barani Ulaya wamempongeza Rais mteule wa Marekani, Donald Trump, kufuatia ushindi wake katika uchaguzi wa rais uliofanyika Jumanne, licha ya wasiwasi mkubwa barani humo juu ya namna muhula wake wa pili utakavyokuwa kwa uhusiano na ukanda huo.

Licha ya Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, kutoanza vyema na timu ya Trump mwezi uliopita baada ya maafisa wa chama chake cha Labour kutoa ushauri wa uchaguzi kwa mpinzani wake, Kamala Harris, kwenye kampeni, Waziri Mkuu Starmer, alikuwa miongoni mwa viongozi wa kwanza wa ulimwengu kumpongeza Trump mapema ya Jumatano.

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz amesema Ulaya inapaswa kutarajia mabadiliko. Baada ya ushindi wa Trump, mjadala umekuwa mkubwa juu NATO na agenda za Ulaya zitakavyo kuwa.