Ukraine yazuia majeshi ya Russia kusonga mbele

UCRANIA-ZELENSKYY-PREMIO

Wakat huo huo waziri wa mambo ya nje wa Russia amesema vikwazo vilivyowekwa na nchi za Magharibi na usafirishaji wa silaha unakwamisha mazungumzo, Radio Freedom Europe /Radio Liberty imeripoti.

Majeshi ya Ukraine yamepambana Jumamosi kuizua Russia kusonga mbele upande wa kusini na mashariki na nchi, ambako Kremlin inataka kuuteka mkoa wa viwanda wa Donbas. Wachambuzi wa kijeshi wa Magharibi walisema mashambulizi ya Moscow yanakwenda kwa kasi ya pole pole kuliko vile ilivyopangwa.

Wakati Russia ilidai Jumamosi kuwa imeshambulia zaidi ya malengo 380 kwa usiku mmoja huku ikijaribu kupata udhibiti kamili wa maeneo ya Luhansk na Donetsk katika mkoa wa mashariki wa Donbas nchini Ukraine, Viongozi wa Majeshi ya Ukraine wamesema juhudi za jeshi la Russia kuyakamata maeneo kadhaa "hazikufanikiwa -- vita inaendelea.”

Mji wa pili kwa ukubwa wa Ukraine, Kharkiv, umeripotiwa ulilengwa kwa makombora na mizinga Jumamosi.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alisema katika hotubakwa njia ya televisheni Ijumaa usiku kuwa majeshi ya Ukraine yamekidhibiti tena kijiji muhimu cha kimkakati karibu na mji huo na kuwaondoa mamia ya raia.

Wito kutoka Rome

Wakati huo huo Umoja wa Mataifa unaendelea kusimamia mashauriano ya kuondolewa raia kutoka katika eneo lililoharibiwa sana la Mariupol, mji wa kusini wa bandari ambao Russia inataka kuuteka tangu uvamizi dhidi ya Ukraine ilipoanza zaidi ya wiki tisa zilizopita.

Wanawake wawili wa Ukraine ambao waume zao wanapigana kukilinda Kiwanda cha chuma cha Azovstal kilichozingirwa huko Mariupol wamewasili Rome Ijumaa, wakisema uokoaji wa raia uwahusishe kuwaondoa takriban wanajeshi 2,000 waliokwama katika kiwanda hich0, ambacho ni ngome ya wapiganaji wa Ukraine wanaoulinda mji huo wa bandari na hivi sasa umeharibiwa kwa mabomu kabisa.

Wameeleza kuwa hofu yao ni kuwa wanajeshi hao watateswa na kuuawa kama wataachwa nyuma na kutekwa na majeshi ya Russia.