Ukraine, inatarajia kupokea mwitikio mzuri kutoka Umoja wa Ulaya kwa maendeleo yake ya kupata uwanachama wa Umoja wa Ulaya (EU), naibu waziri mkuu wa Ukraine, Olha Stefanishyna, ameiambia Reuters, Jumatatu.
Stefanishyna, amesema Kyiv, imetekeleza mageuzi yote yaliyohitajika.
Inatarajia repoti ya Jumatano ijayo itatoa ishara ya mwanzo wa mazungumzo ya Ukraine, kuingia EU kuanzia mwezi Desemba.
Uanachama wa EU unachukuwa miaka mingi kuupata, ambapo mwombaji anatakiwa akamilishe vigezo vikali vya kisheria, na kiuchumi kabla ya kujiunga.
EU ambayo ina nchi wanachama 27, haipo tayari kutoa uanachama kwa nchi iliyopo vitani.
Poland, ambayo ni mwanachama wa EU, waendesha malori wake walifunga mipaka mitatu na Ukraine, Jumatatu, wakipinga kushindwa kwa serekali kulinda biashara kutokana na ushindani wa wageni toka kuanza kwa uvamizi wa Russia nchini Ukraine.