Rais wa Ukraine, Volodomyr Zelenskyy, amesema katika hotuba yake ya kila siku Alhamisi usiku kwamba maandalizi ya mashambulizi ya Russia yameonekana karibu na kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia cha Ukraine, ambacho ni kikubwa kote barani Ulaya.
Rais Zelensky amesema hakuna yoyote ambaye alitumia kinu cha nyuklia kutishia ulimwengu wote, na kwamba pande zote duniani lazima ziwajibike kuzuia uvamizi wa eneo la kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia.
Hii ni maslahi ya dunia na si Ukraine peke yake alisema.
Ukraine na Russia zinalaumiana kuhusiana na hali ya kujipanga kwa mashambulizi katika kinu hicho cha nyuklia.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Antonio Guterres, amesema katika taarifa yake kwamba kinu hicho kisitumike kama sehemu ya oparesheni za kijeshi.
Ameongeza kusema kwamba makubaliano ya haraka yanahitajika ili kuwepo na usalama wa eneo hilo.