Ukraine yataka Russia kukabwa zaidi

Harakati za uchaguzi wa eneo la Ukraine la Donetsk.

Ukraine imetoa mwito kwa mataifa yanayo iunga mkono kuweka wazi kwa Russia kwamba majaribio yake ya unyanyasaji, vitisho, na majaribu yataongeza zaidi uungwaji mkono kwa Ukraine.

Huungwaji mkono huo ni katika mgogoro ambao umeanza Febuari baada ya Russia kuivamia Ukraine.

Taarifa ya wizara ya mambo nje ya Ukraine inaeleza kuwa inatoa mwito kwa Umoja wa Ulaya, NATO na kundi la mataifa saba kuongeza msukumo wa haraka kwa Russia.

Msukumo huo unajumuisha kuweka vikwazo vipya vikali na kuongeza misaada yao muhimu ya kijeshi ikijumuisha kuipatia vifaru, ndege za mapambano, magari ya kivita, makombora ya masafa ya mbali, na kutungua ndege pamoja na mifumo ya kujizuia na mamkombora.

Mwito huo umetolewa baada ya Russia kufanikiwa kuweka viongozi wanaoiunga mkono katika maeneo ya Luhansk na Kherson leo hii.