Shambulizi hilo limesababisha foleni ndefu ya magari baada ya kuelekezwa katika njia tofauti, kulingana na taarifa ya maafisa walioteuliwa na Russia iliyotolewa Alhamisi.
Njia hiyo inayojulikana kama “ lango la kuingia Crimea” ni mojawapo ya njia chache kati ya Crimea, ambayo Moscow ilinyakuwa kutoka Ukraine mwaka 2014 na Ukraine bara.
Iko kwenye njia inayotumika na jeshi la Russia kusafiri kati ya Crimea na maeneo mengine ya Ukraine chini ya udhibiti wake.
Shirika la habari la RIA liliripoti kwamba Wachunguzi wa Russia walisema kuwa makombora manne yalirushwa na wanajeshi wa Ukraine kwenye daraja hilo.
RIA imemnukuu msemaji wa wachunguzi wa kijeshi akisema kuwa alama zilizopatikana kwenye mabaki ya mojawapo ya makombora hayo zinaonyesha kuwa zilitengenezwa nchini Ufaransa.
Ukarabati wa daraja la Chonhar unaweza kuchukua hadi wiki kadhaa, afisa wa wizara ya ya usafiri ya Russia huko Crimea amesema leo.